Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 14, 2016

Kesha la Asubuhi,Jumamosi na Jumapili,Agosti 2016

Agosti 20                        Kristo Ndiye Njia Yetu                        Pekee Kumfikia Baba Naye,kwa sababu hii , aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwayeye; maana yu hai siku zote i l i awaombee. Waebrania 7:25.         Mungu anapatanishwaje na watu? — Kwa kazi na ustahilifu wa Yesu Kristo, ambaye aliondooa kila kitu ambacho kingeingia kati ya mwanadamu na upendo wa Mungu unaosamehe. Sheria ambayo mtu ameivunja haibadilishwi ili kumfikia mwenye dhambi katika hali yake ya anguko katika dhambi, lakini imedhihirishwa kama nakala ya tabia ya Yehova, -- mwakilishi wa mapenzi ya mtakatifu, -- na inatukuzwa na kukuzwa katika maisha na tabia ya Yesu Kristo.Licha ya hivyo, njia ya wokovu imetolewa; kwani Mwãna-Kondoo wa Mungu ...

Lesson jumamosi na Jumapili,Agost 2016

Picha
 Somo la 9                                                                                   Agosti 20—26 Yesu Alihudumia Mahitaji Yao Usomaji wa Biblia: Ezra 3 Sabato Mchana Soma kwa Ajii ya Somo la Juma Hili: Marko 5:22-43; 10:46-52; Yohana 5:1-9; Zaburi 139:1-13:, Marko 2:1-12; Mdo. 9:36-42. Fungu la Kukariri: Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji,akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme,na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. (Mathayo 9:35). M wananamke Mwadventista aliyekuwa amestaafu kazi k...

Usomaji wa Biblia kwa mpango Agosti 21,2016

Ezra 4 1  Basi adui za Yuda na Benyamini, waliposikia ya kuwa wana wa uhamisho wanamjengea Bwana, Mungu wa Israeli, hekalu,  2  wakamkaribia Zerubabeli, na wakuu wa mbari za mababa, wakawaambia, Na tujenge sisi nasi pamoja nanyi; kwa maana tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi, nasi twamtolea dhabihu tangu zamani za Esar-hadoni, mfalme wa Ashuru, aliyetupandisha mpaka hapa.  3  Lakini Zerubabeli, na Yoshua, na wakuu wengine wa mbari za mababa katika Israeli, wakawaambia, Ninyi haiwahusu kushirikiana nasi katika kumjengea Mungu wetu nyumba; bali sisi wenyewe peke yetu tutamjengea Bwana, Mungu wa Israeli, nyumba, kama mfalme Koreshi, mfalme wa Uajemi, alivyotuamuru.  4  Ndipo watu wa nchi wakaidhoofisha mikono ya watu wa Yuda, wakawasumbua, walipokuwa wakijenga.  5  Wakawaajiri washauri juu yao, ili kuwapinga kusudi lao, siku zote za Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata wakati wa kutawala kwake Dario, mfalme wa Uajemi.  6  Tena, wakati wa kut...

Usomaji wa Biblia kwa mpango Agosti20,2016

Ezra 3 1  Hata ulipowadia mwezi wa saba, na wana wa Israeli walipokuwa katika miji yao, watu wakakusanyika pamoja huko Yerusalemu kama mtu mmoja.  2  Ndipo akasimama Yoshua, mwana wa Yosadaki, na ndugu zake makuhani, na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na ndugu zake, nao wakaijenga madhabahu ya Mungu wa Israeli, ili kutoa sadaka za kuteketezwa juu yake, kama ilivyoandikwa katika torati ya Musa, mtu wa Mungu.  3  Wakaiweka madhabahu juu ya msingi wake; maana hofu imewashika kwa sababu ya watu wa nchi; wakamtolea Bwana sadaka za kuteketezwa juu yake, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni.  4  Wakaishika Sikukuu ya Vibanda, kama ilivyoandikwa, wakatoa sadaka za kuteketezwa za kila siku kwa hesabu yake, kama ilivyoagizwa, kama ilivyopasa kila siku;  5  na baadaye sadaka ya kuteketezwa ya daima, na za mwandamo wa mwezi, na za sikukuu za Bwana, zilizoamriwa na kuwekwa wakfu, na za kila mtu aliyemtolea Bwana sadaka kwa hiari yake.  6 ...