Lesson Agosti 27-Sept 2,2016

Somo la 10 Agosti 27 — Septemba 2 Yesu Aliwafanya Wamwamini Usomaji wa Biblia: Ezra 10 Sabato Mchana Soma kwa Ajili ya Somo la Juma Hili: Mwa. 15:6; Hes. 11:4; 1 Kor. 3:1-9; Dan. 6:1-3; Neh. 2:1-9; Kum. 4:1-9; Mdo. 2:42-47. Fungu la Kukariri: “Lakini habari zake zikazidi kuenea, wakakutanika makutano mengi wamsikilize na kuponywa magonjwa yao.” (Luka5:15). K wa miaka kadhaa, Kanisa moja la Waadventista wa Sabato limekuwa likitoa kifungua kinywa siku tano kwa juma kwa shule ya awali ya mahali pale. Ijapokuwa serikali ya taifa lile ilikuwa ya kiraia kabisa (haikuwa ya kidini), ililazimika kupitisha sheria ili kutoa pesa ya kutosha k...