januari28-Talanta Zilizotumiwa Vibaya
Talanta Zilizotumiwa Vibaya Na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo ndiye baba yao wapigao kinubi na filimbi. Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma. Mwanzo 4:21, 22. Kwenye Gharika uvumbuzi Wa sanaa na ustadi wa binadamu ulioangamia ulikuwa wa juu kuliko dunia inavyojua leo. Sanaa iliyoangamizwa ilikuwa zaidi ya sanaa inayofikiria ambayo ulimwengu unajivunia leo. ... Alipokuwa akiuangalia ulimwengu, Mungu aliona kwamba akili aliyokuwa amewapa watu ilikuwa imepotoshwa, kwamba fikra za moyo wake zilikuwa ovu wakati wote. Mungu alikuwa amewapatia watu hawa ujuzi. Alikuwa amewapatia mawazo ya thamani, ili wapate kukamilisha mpango wake. Lakini Bwana aliona kuwa wale aliowaumba ili wawe na hekima, busara na uamuzi, walikuwa wakitumia kila uwezo wa akilj zao kutukuza nafsi. Kwa kutumia maji ya Gharika, alifutilia mbali jamii hii iliyokuwa ikiishi muda mrefu kutoka katika dunia na pamoja nao ukaangamia ujuzi amba...