Ufunuo wa Yohana

Kulikuwa na Vita Mbinguni;Mikaeli na Malaika zake wakapigana na yule joka,yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;nao hawakushinda,wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa,nyoka wa zamani,aitwaye ibilisi na shetani,audanganyaye ulimwengu wote;akatupwa hata nchi,na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Nikasikia sauti kuu mbinguni,ikisema,Sasa kumekuwa wokovu,na nguvu,na ufalme wa Mungu wetu,na mamlaka ya Kristo wake;kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu,yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.Nao wakamshinda kwa damu ya mwana kondoo,na kwa neno la ushuhuda wao,ambao hawakuyapenda maisha yao hata kufa. Kwa hiyo shangilieni,enyi mbingu,nanyi mkaao humo.Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu ny...