Januari 22- Alitembea Pamoja na Mungu
Alitembea Pamoja na Mungu Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu. Mwanzo 5:21, 22. Kuhusu Henoko imeandikwa kwamba aliishi miaka sitini na mitano, akazaa mwana... Katika miaka hii ya awali Henoko alikuwa amempenda na kumcha Mungu na alikuwa amezishika amri zake... Lakini baada ya kuzaliwa kwa mwana wake wa kwanza, Henoko alifikia kiwango cha juu zaidi cha uzoefu; alivutwa kuwa katika uhusiano wa karibu zaidi na Mungu. Kwa ukamilifu zaidi alitambua majukumu yake binafsi na wajibu kama mwana wa Mungu. Alipoona upendo wa mwana kwa baba yake, usahili wake wa kutegemea ulinzi wake; alipojisikia upendo wenye shauku, wenye kina uliotoka moyoni mwake kwa ajili ya mwana wake wa kwanza, aljifúnza somo la pekee la upendo wa ajabu wa Mungu kwa watu katika karama ya Mwana wake na ujasiri ambao watoto wa Mungu wanaweza kuwa nao katika Baba yao wa r...