Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba 25, 2016

Kuwahubiri wauaji Sehemu ya II-Somo toka Rwanda

Picha
Na Fodidas Ndamyumugabe Kumbuka: Fodidasi amekamatwa na wauaji, waliomwamuru ajichimbie kaburi lake mwenyewe. Kadri aliyochimba kaburi, mmoja wa wauaji hao alivutiwa na Biblia ya Fodidasi na kuanza kumwuliza maswali. Mara baada ya kaburi kuchimbwa ,kundi hilo la wauaji liliamua kutumia kaburi hilo kumzika mtu mwingine. Kabla ya kumwamuru Fodidasi kuchimba kaburi la pili, walimpatia wasaa apate kuwahubiri. Kwanza ninawashukuru sana. “Ahsanteni kwa kufanya dua kwa ajili ya mtu mliyemwua. Hata hivyo mwapaswa mjue Biblia isemacho kuhusu kifo—wasaa pekee ambapo waweza kuokolewa ni wakati ukingali hai—siyo baada ya kifo. “ Kwa sababu walio hai wanajua kuwa watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote ” Mhubiri 9:5. “Sitawasihi kuwa mniachie hai,” aliendelea kujieleza, “kwa sababu najua hata mkiniua muda utafika ambapo nitafufuliwa.” “Miongofli mwa watu mnaowaua ni wa makabila mengine—siyo Wahutu au Watusi. Ni watoto wa Mungu. Mnafikiri mnapambana vita ya kikabila, ila mmekosea. H...

Kuwahubiri wauaji -Sehemu ya Kwanza

Picha
somo toka Rwanda Na  Fodidas Ndamyumugabe Kisa cha  msamaha na kusameheana kwa wahanga wa mauaji wa kimbari nchini Rwanda yaliyotokea mwaka 1994. Ni matukio halisi, yenye kusikitisha na kuvuta hisia kwa kiasi kikubwa.          Fodidasi-ambaye jina lake humaanisha “Ninamwabudu BWANA” alizaliwa katika kaya ya Kiadventista  iliyokuwa ikiishi milimani huko Rwanda. Tangia ujana wake  alionesha kuwa ana kipaji cha uongozi, akajitoa kumtumikia Bwana. Alikuwa na bidii katika chama cha Watafuta njia na hatimaye katika chama cha Vijana. Alikuwa mlezi mwema wa kiroho wa vijana wenzake ,na kuongoza ibada asubuhi shuleni mwao kila siku.          Kadiri miaka ilivyosogea Biblia yake ilikuwa imepigiwa mistari kila mahali kuonesha aliisoma kwa bidii. Fodidasi hakujua ni kwa jinsi gani Biblia hiyo itaokoa maisha yake mnamo vita vya kimbari mwaka 1994 pale alipohitajika kuwahubiri Wauaji. K...