Kesha la Asubuhi Agost 13- 19 ,2016
Agosti 13 Inatupasa Tusionee Fahari Watu Na tena, Bwana anayafahamu mawazo ya wenye hekima ya kwamba ni ya ubatili Basi, mtu ye yotee na asijisifie wanadamu. 1 Wakorintho 3 :2 0,21. Tunaishi katika kipindi cha upotovu na wanaume kwa vijana ni jasiri katika dhambi. Vijana wetu wasipolindwa kwa utakatifu, wasipolindwa kwa kanuni thabiti, uangalizi mkubwa usipodhihirishwa katika kuchagua rafiki zao pamoja na machapisho yanayolisha akili, watakuwa wameachiliwa kwa jamii ambayo maadili yao yamechafuka kama yalivyokuwa ya wakazi wa Sodoma... Vijana wetu watakutana na majaribu kila upande na ni lazima waelimishwe kwamba itawapasa wategemee nguvu itokayo juu, mafundisho kutoka juu, kuliko yale yatolewayo na binadamu. Kila mahali wapo wale wanaomdharau Bwana wetu, ambao kwa mazoea hubeza Ukristo... Wale wasio na nguvu ya kimaadili hawawezi kusimama kidete kulinda ukweli; hawana ujasiri wa kusema: “Mazungumzo ya namna hiyo yasipokoma, siwezi kusalia hapa pamoja nawe....