Somo 8:Yesu Alionesha Huruma Agosti 13-19,2016
Yesu
Alionesha Huruma
Usomaji wa Biblia: 2 Nyakati 32Agosti 13
Sabato Mchana
Kinyume na wazo la watu wengi kuwa Mungu wa Agano la Kale ni mkali,bahili, asiyesamehe na asiye na huruma hasa unapomweka kinyume na Yesu na jinsi anavyoelezewa katika Agano Jipya, hizi ni baadhi tu ya aya nyingi za Agano la Kale zinazoifunua huruma ya Mungu kwa wanadamu.
Soma Mathayo 9:35, 36 na Luka 7:11—16. Mafungu haya yanatufundisha nini kuhusu jinsi zilivyo kweli huruma na upole unaodhihirishwa?
Usomaji wa Biblia: 2 Nyakati 32Agosti 13
Sabato Mchana
Soma kwa Ajili ya Sorno la Juma Hill: 2 Fal. 13:23; Kut. 2:23—25;
Luka 7:11-16; 1 Yoh. 3:17; Yn. 11:35; Rum. 12:15; 2 Kor. 1:3,4.
Fungu la Kukariri: “Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia,
akawaponya wagonjwa wao.” (Mathayo 14:14).
Lingekuwa jambo la kusikitisha kiasi gani? Msichana mwenye umri wa miaka 17 alikuwa anapambana na kile ambacho wasichana wengi wa umri
huo hupambana nacho, lakini zaidi sana, msichana huyo alijinyonga. Nani
angeweza kukisia huzuni kubwa iliyokuwa imewafikia wazazi wake?
Mchungaji aliitembelea nyumba ile. Aliketi sebuleni jirani tu nao na kwa kitambo alikuwa amenyamaza. Alijiunga na kuzama katika huzuni waliyokuwa nayo. Baadaye mchungaji huyu alianza kulia kwa sauti. Alilia kwa sauti mpaka machozi yake yakamkauka. Bila ya kusema neno lo lote, mchungaji alisimama na kuondoka. Siku kadhaa baadaye, baba wa binti aliyekuwa amekufa alimshukuru mchungaji kwa kile alichokuwa amekifanya. Kwa wakati ule wa msiba, yeye na mke wake hawakuwa wanahitaji maneno, ahadi ama ushauri nasaha. Walichokuwa wanahitaji sana kwa wakati huo, ni kuhurumiwa.
“Sina maneno ya kueleza,” alimwambia mchungaji, “jinsi huruma yako
ilivyokuwa na maana kwetu wakati ule.”
Neno la Kiingereza ‘sympathy ‘ linalotafsiriwa kuwa huruma maana yake ni kuwa na ‘pathos’ neno lingine la Kiingereza limaanishalo hali ya kusababisha hisia za huruma au huzuni na neno ‘pathos ‘ linahusiana na kusikitikia, kuwa mpole kwa, na kuhuzunikia. Kuonesha huruma katika majonzi ya watu wengine huchukua suala la “kuchanganyika” nao katika daraja jipya kabisa.
Kuonesha huruma pia ilikuwa ni njia muhimu aliyokuwa anaitumia Yesu kuwafikia watu.

* Soma sorno lajuma hili ukijiandaa kwa ajili ya Sabato ya Agosti 20
Jumapili
Usomaji Wa Biblia: 2 Nyakati 33 Agosti 14
Kusikia Sauti za Kuugua
Ulimwengu huu unaweza kuonekana kuwa mahali pa kutisha mno: ni
mkubwa mno, baridi, na tunahisi kwa kiasi kikubwa sana kule kutokufaa kwetu na kutokuwa na maana yo yote ndani yake. Hofu hii hata imeenea zaidi kutokana na ujio wa sayansi ya kisasa, ambayo kwa sababu ya kuwa na vionambali vyenye uwezo mkubwa vimegundua ulimwengu mwingine
mkubwa na mpana kuliko uwezo wetu wa kuelewa haraka. Na juu ya hayo,
ongezea madai makubwa kupita kiasi ya mafundisho ya Darwin, ambayo
kulingana na matoleo yake maarufu sana, huitupilia mbali dhana ya Mwumbaji,na watu kwa kuelewa, wanaweza kupambana na hali isiyoleta matumaini yoyote katikati ya uumbaji unaoonekana kutokujali kitu cho chote kuhusu sisi.

Kwa kweli, Biblia inatupa mtazamo tofauti
juu ya sehemu yetu katika uumbaji.
Aya zifuatazo hufundisha nini juu ya huruma za Mungu kwa viumbe wake walioanguka na kuvunjika waliomo duniani?
Amu. 2:16—18 _________________________________________________
2 Fal. 13:23 _____________________________________________________
Isa. 54:7, 8, 10 ___________________________________________________

Amu. 2:16—18
|
Waamuzi. 2
16 Kisha Bwana
akawainua waamuzi, waliowaokoa na mikono ya watu hao waliowateka nyara.
17 Lakini hawakuwasikiliza hao waamuzi wao, maana walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine, wakajiinamisha mbele yao; wakageuka upesi, na kuiacha njia ile waliyoiendea baba zao, waliozitii amri za Bwana bali wao hawakufanya hivyo. 18 Na wakati Bwana alipowainulia waamuzi, ndipo Bwana alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo; maana Bwana alighairi kwa ajili ya kuugua kwao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua. |
2 Fal. 13:23
|
Fal. 13
23 Lakini Bwana
akawahurumia, akawasikitikia, na kuwaangalia, kwa ajili ya agano lake na
Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, wala hakutaka kuwaangamiza, wala hakuwatupa
usoni pake bado.
|
Isa. 54:7, 8, 10
|
Isaya 54
7 Kwa kitambo kidogo
nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya.
8 Kwa ghadhabu ifurikayo nalikuficha uso wangu dakika moja; lakini kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema Bwana, Mkombozi wako. 9 Kwa maana jambo hili limekuwa kama maji ya Nuhu kwangu; maana kama nilivyoapa ya kwamba maji ya Nuhu hayatapita juu ya dunia tena, kadhalika nimeapa ya kwamba sitakuonea hasira, wala kukukemea. 10 Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema Bwana akurehemuye. |
Kinyume na wazo la watu wengi kuwa Mungu wa Agano la Kale ni mkali,bahili, asiyesamehe na asiye na huruma hasa unapomweka kinyume na Yesu na jinsi anavyoelezewa katika Agano Jipya, hizi ni baadhi tu ya aya nyingi za Agano la Kale zinazoifunua huruma ya Mungu kwa wanadamu.
Kutoka 2 : 23—25 hutufundisha
nini kuhusu jinsi Mungu anavyoshu
ghulika na mateso?
ghulika na mateso?
Kutoka 2 : 23—25
|
Kutoka 2
23 Hata baada ya siku
zile nyingi mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule
utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa.
24 Mungu akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na Isaka na Yakobo. 25 Mungu akawaona wana wa Israeli, na Mungu akawaangalia. |
Yakobo 5:11
|
Yakobo 5
11 Angalieni, twawaita
heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa
Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.
|
Mungu huwajali sana watu (angaliaYakobo 5:11). Hii ni mada iliyoonekana katika
Biblia yote.
“Moyo wake wa upendo unaguswa na masikitiko yetu na hata kwa kuyataja kwetu. . . Hakuna jambo lo lote linalohusu amani yetu kwa namna fulani,linakuwa ni dogo sana kiasi kwamba asiweze kulitambua. . . Hakuna janga linaloweza kuwapata wadogo kabisa kati ya watoto wake . . . ambalo Baba yetu wa mbinguni si msikivu kwalo, au ambalo hawezi kuvutwa kwalo mara moja.” Ellen G. White, Steps to Christ, uk. 100.

Ni kuugulia kupi kwa pamoja
kunapanda juu kwenda mbinguni
kutoka katika jamii yako, na Mungu atakutumiaje kuwahurumia na kuwasaidia wanaoteseka? |
Jumatatu Usomaji Wa Biblia: 2 Nyakati 34 Agosti 15
Mwokozi Wetu Mwenye Huruma
Kwa kadiri Yesu alivyochangamana na watu wakati wa huduma yake duniani, alikutana na mazingira yaliyoifunua huruma na upole wake kwao.
“Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia akawaponya wagonjwa wao.” (Mat. 14:14).
Kwa kadiri Yesu alivyochangamana na watu wakati wa huduma yake duniani, alikutana na mazingira yaliyoifunua huruma na upole wake kwao.
“Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia akawaponya wagonjwa wao.” (Mat. 14:14).
Soma Mathayo 9:35, 36 na Luka 7:11—16. Mafungu haya yanatufundisha nini kuhusu jinsi zilivyo kweli huruma na upole unaodhihirishwa?
Mathayo 9:35, 36
|
|
Mathayo 9
35 Naye Yesu alikuwa
akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na
kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila
aina.
36 Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji. |
|
Luka 7:11—16
|
|
Luka 7
11 Baadaye kidogo
alikwenda mpaka mji mmoja uitwao Naini, na wanafunzi wake walifuatana naye
pamoja na mkutano mkubwa.
12 Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wa mjini wengi walikuwa pamoja naye. 13 Bwana alipomwona alimwonea huruma, akamwambia, Usilie. 14 Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka. 15 Yule maiti akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake. 16 Hofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu; na, Mungu amewaangalia watu wake. |
Neno huruma huleta pia
akilini mwa mtu maneno mengine yanayohusiana nalo, kama vile maneno ya
Kiingereza ‘empathy’ linalomaanisha uwezo wa kuelewa hisia za wengine na ‘pity’
lenye maana ya sikitiko. Kulingana na kamusi mbalimbali, upole ni sikitiko, huruma,
kuelewa hisia za wengine.Sikitiko ‘pity’ni huzuni yenye kuhurumia mateso ya mtu
mwingine. ‘empathy’ ni uwezo wa kuelewa ama kuzishiriki hisia za watu wengine.
Upole na huruma huonesha kuwa siyo tu tunatambua kinachowaumiza wengine lakini
kwamba tunahitaji kusaidia kupunguza ama kuyaponya na maumivu hayo.
Pale unaposikia jambo la kuhuzunisha ambalo limetokea kwa watu katika jamii yako, kama vile kuunguliwa nyumba ama kifo katika familia, unaitikiaje?Je, unaishia kusema kichini chini kwamba, “Jambo hilo linahuzunisha sana,”halafu unaendelea na shughuli zako, jambo ambalo ni rahisi kufanya? Au huruma yako huamshwa na kukufanya kwa upole utake kuwahudumia? Upole na huruma ya kweli itakuongoza kuwafariji na kwa bidii kuwasaidia marafìki na wageni pia kwa vitendo ama iwe kwa njia ya kuwatumia kadi kuwatia moyo ama kuonesha huruma ya kina kwa kuwatembelea na kuwasaidia katika mahitaji yao ya wakati ule, tendo la upendo ni matokeo ya wazi ya huruma ya kweli.
Kwa bahati nzuri, watu na mashirika ya kutoa misaada wanaelekea kuitikia wakati wa maafa makubwa. Hata hivyo, wakati mwingine inawezekana tusiyaangalie kwa uzito unaostahili matatizo na balaa “ndogo ndogo” zjnazomsumbua mno mtu fulani. Yesu hakuishia tu kuonesha huruma lakini aliichukua huruma hiyo kwenda katika ngazi nyingine: tendo la kuhurumia.Sisi, kwa kweli, tumeitwa kufanya vivyo hivyo. Mtu ye yote anaweza kujisikia sikitiko au huruma kwa mwingine aliyekumbwa na matatizo. Swali ni kwamba huruma inatuongoza kuchükua hatua gani?
Walipokuwa mezani kwa ajili ya kifungua kinywa, mwanamume mmoja alikuwa akimsikiliza mkewe aliyekuwa anasoma habari za maafa yaliyokuwa yameipata nchi nyingine na kusababisha elfu kadhaa za watu kufa. Baada ya maongezi mafupi kuhusu namna janga hilo lilivyokuwa baya, alibadilisha mazungumzo na kuuliza ikiwa timu ya soka ya mahali pale ilikuwa imeshinda mechi yao ya usiku uliopita.

Ni kwa vipi sisi sote kwa
namna fulani tuna hatia kuhusu jambo hili,na ni kitu gani tufanye, kama kipo,
kuhusiana na hili?
|
Jumanne Usomaji wa
Biblia: 2 Nyakati 35 Agosti 16
Kupitia Uzoefu Wao
Soma Wakolosai 3:12, 1 Petro
3:8 na 1 Yohana 3:17. Aya hizi zinatuainbia nini, na tutaidhihirishaje huruma
hii maishani mwetu?
____________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________
____________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________
Wakolosai 3:12
|
Wakolosai 3
12 Basi, kwa kuwa
mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu
wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,
|
1 Petro 3:8
|
1 Petro 3
8 Neno la mwisho ni
hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu,
wasikitikivu, wanyenyekevu;
|
1 Yohana 3:17
|
1 Yohana 3
17 Lakini mtu akiwa na
riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma
zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?
|
Huruma ni neno linalotokana na neno la Kilatini compati, lenye maana ya “kuteseka
pamoja na.” Kama ambavyo sisi wenyewe tumeteseka, kwa hiyo pia tunaweza
kuyaelewa mateso ya watu wengine, na, bila shaka; kama ambavyo sisi
tunavyotamani kuhurumiwa katika mateso yetu, ni lazima tuwe tayari kufanya
vivyo hivyo pia kwa wengine katika uhitaji wao.
Katika somo lililotangulia, tuliona kisa cha Msamaria mwema.Anapousisitiza mfano wa Msamaria, Yesu anasema, “Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia (Luka 10:33). Huruma hii ilimsukuma Msamaria aliyekuwa anasafiri kuchukua hatua kwa niaba ya aliyekuwa amejeruhiwa. Inawezekana kuhani na Mlawi walijiuliza swali hili kila mmoja wao, “Nitakapomsaidia mtu huyu,nini kitanipata?” Na inawezekana pia Msamaria alijiuliza swali hili, “Kama sitamsaidia mtu huyu, kitu gani kitampata?” Katika kisa hiki Msamaria bila ubinafsi wo wote, anaangalia kwa jicho la mbali kitakachompata mhanga wa matatizo na kuchukua hatua. Alihatarisha usalama na alivyokuwa navyo kwa ajili ya mgeni yule. Kwa maneno mengine, kuwa Mkristo mara zingine huambatana na hatari na inaweza kuwa na gharama kubwa sana inayongojea.
Angalia kisa cha mwana mpotevu kwa mtazamo kama huu huu pia (Luka15 :20—32). Baba wa mwana mpotevu alifanya jambo gani lililomfanya afùngue mlango wa kukosolewa na familia kutoelewana? Kukumbatia kwa moyo wa huruma, joho la kutambuliwa kama mwana familia, pete ya kuaminiwa, viatu vya uhuru na kuitishwa kwa sherehe kunaakisi furaha isiyo na ubinafsi ya Baba ambaye alikuwa tayari kutoa vyote kwa ajili ya urejeshwaji wa mwanawe aliyekuwa amepotea. Mpotevu maana yake ni mfujaji, asiyejali, mbadhirifu,na asiyejitawala. Aina hii ya tabia kwa hakika inaelezea njiia aliyoipitia mwana katika kisa hiki. Hebu tulia na utafakari kwamba, kwa mwitikio wa kurudi kwa mwana mpotevu, mtu fulani angeweza kudai kwa haki kuwa baba katika kisa hiki anaweka pembeni heshima yake na bila kujali cho chote anatoa kila kitu alicho nacho kwa mwanawe mchafu. Machoni pa ndugu mkubwa,baba ni mfujaji, mbadhirifu, na asiyeweza kujitawala. Baba anakuwa mpotevu machoni pa mwanawe aliyetubu, na moyo wake wa huruma unachochea utoaji wa hazina zote zilizokuwa zinalazimika kutumika ili kumrejesha.
Ngazi hii ya huruma inahusisha kuweka nafsi kando, na inaweza kutuweka katika hatari kwa lo lote litakalokuja pale tutakapokuwa tunateseka pamoja na mtu fulani na kujitahidi kuwasogeza katika kurejeshwa upya. Kwa kifupi,upole na huruma ya kweli inaweza kuja na gharama.

Jumatano Usomaji wa Biblia: 2 Nyakati 36 Agosti 17
Yesu Akalia Machozi
“Yesu akalia machozi “
(Yohana 11:35). Aya hii inatuambia nini, si tu kuhusu ubinadamu wa Yesu, bali
ni kwa vipi katika ubinadamu huo
alijihusisha na mateso ya wengine? angalia pia Rum. 12:15.
alijihusisha na mateso ya wengine? angalia pia Rum. 12:15.
Yohana 11:35
|
Yohana 11
33 Basi Yesu
alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua
rohoni, akafadhaika roho yake,
34 akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame. 35 Yesu akalia machozi. |
Rum. 12:15
|
Warumi 12
15 Furahini pamoja nao
wafurahio; lieni pamoja nao waliao.
|
Katika Yohana 11:35 Yesu alionesha huruma,
aliweza kutambua hisia za watu na alikuwa na huzuni ya kutoka ndani ya moyo
wake. Ingawaje alikuwa karibu kumfufua Lazaro kutoka katika wafu, huzuni ya
familia aliyokuwa karibu sana nayo ilimwathiri kimwili na kimhemko.
Hata hivyo, Yesu alikuwa halii tu kwa sababu ya kifo cha rafiki yake
kipenzi, alikuwa anaangalia suala kubwa zaidi, lile la mateso ya wanadamu
wote kwa sababu ya uharibifu mkubwa wa dhambi.
“Uzito wa huzuni ya vizazi vyote ulikuwa juu yake. Aliyaona madhara ya
kuogofya ya uasi dhidi ya sheria ya Mungu. Aliona kuwa katika historia ya
ulimwengu huu, kuanzia kwenye kifo cha Habili, pambano kati ya wema na
uovu limekuwa endelevu. Alipokuwa anaiangalia miaka ijayo, aliona mateso na huzuni, machozi na kifo, ambayo ndiyo yangekuwa sehemu ya maisha ya wanadamu. Moyo wake ulichomwa na maumivu ya jamaa yote ya wanadamu wa vizazi vyote na wa nchi zote. Ole wa jamaa ya wanadamu wenye dhambi ulikuwa mzito na kuuelemea moyo wake, na chemchemi ya machozi yake ilifunguka na kububujika pale alipouwa akitamani sana kuwaondolea mateso yao yote.”—Ellen G. White, The Desire ofAges, uk. 534.
Hebu fikiria maneno yake: Katika njia ambazo hapana mtu hata mmoja
miongoni mwetu angeliweza, [Yesu] aliona “maumivu ya jamaa yote ya wanadamu wa vizazi vyote na wa nehi zote.”
Sisi wenyewe kwa shida sana tunaweza kusimama kufikiria juu ya maumivu ya wale tunaowafahamu au wale tulio karibu nao. Halafu ongezea maumivu ya watu wengine tunayoyasoma katika magazeti. Na bado, hapa tunaye Bwana anayejua mambo yote kwa namna tusizojua, akitiririkwa na machozi juu ya huzuni ya jumla ya wanadamu. Mungu pekee ndiye anayejua ukubwa kamili wa ole na huzuni ya mwanadamu. Tungepaswa kuwa wenye shukrani kiasi gani kwamba tunapata kuona huzuni kwa kiasi kidogo mno na kwa uhafifu, na wakati mwingine hata bicho kidogo huonekana ni zaidi ya vile tunavyoweza kustahimili. Fikiria kwa makini uone kile kilichokuwa kinauchochea moyo wa Yesu kwa wakati ule.

Jenerali William Booth,
mwanzilishi wa Jeshi la Wokovu aliwahi
kusema,” ‘Kama hutaweza kuulilia mji, hatutaweza kukutumia.’ “— Rogers S. Greenway and Timothy M. Monsma, Cities : Missions ‘News Frontier (Grand Rapids, Mich.: Baker Pub. Group, 2000) uk. 246. Maneno hayo yanatakiwa kutuambia fini kila mmoja wetu? |
93
Alhamisi Usomaji
wa Biblia: Ezra 1 Agosti 18
Ama Nyingine ya Mfariji
“Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote; atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu.” (2 Kor. 1:3,4). Paulo anatuambia nini hapa kuhusu jinsi ambavyo mateso yetu sisi wenyewe yanavyoweza kutusaidia kufanya kwa ufanisi zaidi kuwaonesha huruma na faraja wale wanaotuzunguka? Ni kwa jinsi gani umepata uzoefu (kama upo) wa maneno haya maishani mwako?
__________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

2 Kor. 1:3,4
|
2 Kor. 1
3 Na ahimidiwe Mungu,
Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote;
4 atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu. |
Hesabu 35
|
Hesabu 35
1 Kisha Bwana akanena
na Musa katika nchi tambarare za Moabu, karibu na mto wa Yordani, hapo
Yeriko, akamwambia,
2 Uwaagize wana wa Israeli wawape Walawi miji wapate mahali pa kukaa, katika milki yao; pamoja na malisho yaliyoizunguka hiyo miji kotekote mtawapa Walawi. 3 Hiyo miji watakuwa nayo ili wakae humo, na malisho watakuwa nayo kwa wanyama wao wa mifugo, na kwa mali zao, na kwa wanyama wao wote. 4 Na yale malisho ya miji mtakayowapa Walawi, ukubwa wake utakuwa tangu ukuta wa mji kupima kiasi cha dhiraa elfu pande zote. 5 Nanyi mtapima hapo nje ya mji upande wa mashariki dhiraa elfu mbili, na upande wa kusini dhiraa elfu mbili, na upande wa magharibi dhiraa elfu mbili, na upande wa kaskazini dhiraa elfu mbili, huo mji ulio katikati. Hayo ndiyo yatakayokuwa kwao malisho ya miji. 6 Na hiyo miji mtakayowapa Walawi, itakuwa miji sita ya makimbilio, mtakayoweka kwa ajili ya mwenye kumwua mtu, ili akimbilie huko; pamoja na hiyo mtawapa miji arobaini na miwili zaidi. 7 Miji yote mtakayowapa hao Walawi jumla yake itakuwa miji arobaini na minane; mtawapa miji hiyo pamoja na malisho yake. 8 Tena katika miji mtakayotoa ya hiyo milki ya wana wa Israeli, katika hao walio wengi mtatwaa miji mingi; na katika hao walio wachache mtatwaa miji michache; kila mtu kama ulivyo urithi wake atakaourithi, atawapa Walawi katika miji yake. 9 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 10 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapovuka mto wa Yordani na kuingia nchi ya Kanaani, 11 Ndipo mtajiwekea miji iwe miji ya makimbilio kwa ajili yenu; ili kwamba mwenye kumwua mtu, pasipo kukusudia kumwua, apate kukimbilia huko. 12 Na hiyo miji itakuwa kwenu kuwa makimbilio, kumkimbia mwenye kutwaa kisasi, ili asiuawe mwenye kumwua mtu, hata atakaposimama mbele ya mkutano ahukumiwe. 13 Na hiyo miji mtakayowapa itakuwa kwenu ni miji sita ya makimbilio. 14 Mtawapa miji mitatu ng'ambo ya pili ya Yordani, na miji mitatu mtawapa katika nchi ya Kanaani; miji hiyo itakuwa ni miji ya makimbilio. 15 Miji hiyo sita itakuwa miji ya makimbilio kwa ajili ya wana wa Israeli, na kwa ajili ya mgeni, na kwa ajili ya huyo aketiye kati yao hali ya ugeni; ili kila amwuaye mtu, naye hakukusudia kumwua, apate kukimbilia huko. 16 Lakini kama alimpiga kwa chombo cha chuma, akafa, ni mwuaji huyo; mwuaji hakika yake atauawa. 17 Na kama alimpiga kwa jiwe lililokuwa mkononi mwake, ambalo kwa hilo humkini mtu kufa, naye akafa, yeye ni mwuaji; huyo mwuaji lazima atauawa. 18 Au kama alimpiga kwa chombo cha mti kilichokuwa mkononi mwake ambacho kwa hicho humkini mtu kufa, naye akafa, ni mwuaji huyo, mwuaji lazima atauawa. 19 Mwenye kutwaa kisasi cha damu ndiye atakayemwua mwuaji; hapo atakapokutana naye, atamwua. 20 Tena kwamba alimsukuma kwa kumchukia, au kwamba alimtupia kitu kwa kumvizia, hata akafa; 21 au akampiga kwa mkono wake kwa kuwa ni adui, naye akafa; yeye aliyempiga lazima atauawa; yeye ni mwuaji; mwenye kutwaa kisasi cha damu atamwua mwuaji, hapo atakapokutana naye. 22 Lakini ikiwa alimsukuma ghafula pasipo kumchukia; au akamtupia kitu cho chote pasipo kumvizia, 23 au kwa jiwe liwalo lote, ambalo kwa kupigwa kwalo humkini mtu kufa, asipomwona, akamtupia hata akafa, naye hakuwa adui yake, wala hakumtakia madhara; 24 ndipo mkutano utaamua kati ya huyo aliyempiga mtu na huyo atakayetwaa kisasi cha damu, kama hukumu hizi zilivyo; 25 nao mkutano utamwokoa yule aliyemwua mtu na mkono wa mwenye kutwaa kisasi cha damu; tena mkutano utamrejeza katika mji wake wa makimbilio, aliokuwa anaukimbilia; naye atakaa humo hata kifo chake kuhani mkuu, aliyepakwa mafuta kwa mafuta matakatifu. 26 Lakini kama mwenye kumwua mtu akienda wakati wo wote kupita mpaka wa huo mji wa makimbilio, alioukimbilia; 27 na mwenye kutwaa kisasi cha damu akamwona, naye yu nje ya mpaka wa mji wake wa makimbilio, na mwenye kutwaa kisasi cha damu akamwua huyo mwuaji, hatakuwa na hatia ya damu; 28 kwa sababu ilimpasa kukaa ndani ya mji wake wa makimbilio hata kifo chake kuhani mkuu lakini kuhani mkuu atakapokwisha kufa huyo mwuaji atarudi aende nchi ya urithi wake. 29 Mambo haya yatakuwa ni amri ya hukumu kwenu, katika vizazi vyenu vyote, katika makazi yenu yote. 30 Mtu awaye yote atakayemwua mtu, huyo mwuaji atauawa kwa vinywa vya mashahidi; lakini shahidi mmoja hatashuhudia juu ya mtu hata akafa. 31 Tena, msipokee fidia kwa ajili ya uhai wa mwuaji, ambaye amekuwa na hatia ya mauti; Lakini lazima atauawa. 32 Tena hamtapokea fidia kwa ajili ya huyo aliyeukimbilia mji wake wa makimbilio, apate kwenda tena kuketi katika nchi, hata kifo cha kuhani mkuu. 33 Hivi hamtaitia unajisi nchi ambayo mwakaa; kwa kuwa damu huitia nchi unajisi; wala hapana sadaka itoshayo kwa ajili ya nchi, kwa ajili ya damu iliyomwagwa ndani yake, isipokuwa ni damu ya huyo aliyeimwaga. 34 Kwa hiyo msiitie unajisi nchi muiketiyo, ambayo naketi nami kati yake; kwa kuwa mimi Bwana nakaa kati ya wana wa Israeli. |
Eze. 47:1—12
|
Eze. 47
1 Baadaye akanileta
tena mpaka lango la nyumba; na tazama, maji yalitoka chini ya kizingiti cha
nyumba, kwa njia ya mashariki, maana upande wa mbele wa nyumba ulielekea
upande wa mashariki; nayo maji yakashuka toka chini ya upande wa kuume wa
nyumba, upande wa kusini wa madhabahu.
2 Ndipo akanileta nje kwa njia ya lango upande wa kaskazini, akanizungusha kwa njia ya nje mpaka lango la nje, kwa njia yake iliyoelekea mashariki; na tazama, maji yalitoka upande wa kuume. 3 Na alipotoka mtu yule, mwenye uzi wa kupimia mkononi mwake, kwenda masharikini, akapima dhiraa elfu, akanivusha maji yale; maji yakafika mpaka viweko vya miguu. 4 Kisha akapima dhiraa elfu, akanivusha maji yale, maji yakafika mpaka magoti. Kisha akapima dhiraa elfu, akanivusha, maji yakafika mpaka viuno. 5 Kisha akapima dhiraa elfu, yakawa mto nisioweza kuuvuka; maana maji yamezidi, maji ya kuogelea, mto usiovukika. 6 Akaniambia, Mwanadamu, je! Umeona haya? Kisha akanichukua akanirudisha mpaka ukingo wa mto. 7 Basi nikiisha kurudi, tazama, kando ya ukingo wa mto ilikuwapo miti mingi sana, upande huu na upande huu. 8 Ndipo akaniambia, Maji haya yanatoka kwenda pande za nchi ya mashariki, nayo yanashuka mpaka Araba, na kuingia katika bahari maji yatokezwayo yataingia baharini ,na maji yake yataponyeka. 9 Tena itakuwa, kila kiumbe hai kisongamanacho, kila mahali itakapofika mito hiyo, kitaishi; kutakuwapo wingi mkubwa wa samaki, kwa sababu maji haya yamefika huko maana maji yale yataponyeka, na kila kitu kitaishi po pote utakapofikilia mto huo. 10 Tena itakuwa, wavuvi watasimama karibu nao; toka Engedi mpaka En-eglaimu, patakuwa ni mahali pa kutandazia nyavu; samaki wao watakuwa namna zao mbalimbali, kama samaki wa bahari kubwa, wengi sana. 11 Bali mahali penye matope, na maziwa yake, hayataponywa; yataachwa yawe ya chumvi. 12 Na karibu na mto, juu ya ukingo wake, upande huu na upande huu, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayatatindika kamwe; utatoa matunda mapya kila mwezi, kwa sababu maji yake yanatoka mahali patakatifu; na matunda yake yatakuwa ni chakula; na majani yake yatakuwa ni dawa. |
Neno la Kiingereza ‘comfort’- faraja, linatokana na neno la Kilatmi corn (pamoja
na) na neno lingine fortis (madhubuti, imara). Kwa kadiri Kristo
anavyotuimarisha katika mateso yetu, tutaupeleka umadhubuti huu kwa
wengine. Kama tulivyojifunza kupitia huzuni zetu, tunaweza kufanya vizuri
zaidi kuwahudumia wengine katika mateso yao. Makanisa kwa ujumla yana
washiriki wanaoteseka na washiriki wanaofariji. Muungano huu unaweza
kubadilisha kanisa lako na kulifanya kuwa “nyumba salama” — “mji wa
makimbilio” (angalia Hesabu 35) na vilevile kuwa mto wa uponyaji (angalia
Eze. 47:1—12) utiririkao na kuingia katika jamii.
Kuonesha huruma na faraja ni sanaa. Hapa kuna baadhi ya mapendekezo:
Kuwa mkweli. Sikiliza zaidi kuliko unavyoongea. Uwe na hakika kuwamwonekano wako (lugha ya mwili) unatia mkazo katika juhudi zako za kuonesha huruma na faraja.
Onesha huruma yako mayotokana na utu wako binafsi. Baadhi ya watu
huonesha huruma kwa kulia kimya kimya na mtu mwenye tatizo. Wengine
huwa hawalii isipokuwa huonesha huruma kwa kupanga kitu Fulani ambacho kitakuwa faraja kwa walio na msiba.
Mara nyingi kuwapo pale ni muhimu kuliko kusema ama kutenda.
Waruhusu watu kuhuzunika katika namna zao.
Zifahamu vizuri hatua za mchakato wa huzuni wanaoupitia watu.
Uwe mwangalifu usije ukasema “ninajua unavyojisikia.” Uwezekano
uliopo ni kwamba hujui.
Kuna nafasi ya ushauri nasaha kwa weledi.
Usiseme “ nitakuombea” isipokuwa una nia hasa ya kufanya hivyo kwa
ajili ya mtu aliye matesoni. Kama ikiwezekana, omba naye, mtembelee bila
kuwa na haraka yo yote, na soma pamoja naye ahadi za Biblia zinazotia moyo.
Panga vikundi vya kusaidia (kama vipo) kutoka kanisani kwako au katika jamii yako.

Ijumaa Usomaji Wa Biblia: Ezra 2 Agosti 19
Tafakari Zaidi: Soma Kum. 24:10—22; Yon. 3; Mal. 3:17; Mat 15:32—38; Mk.
6:34—44;Gal. 6:2; Ebr. 10:32—34; katika Ellen G. White, “Be Sympathetic to All
Men,” uk. 189,na “Thoughtful of Others,” uk. 193, kwenye kitabu kinachoitwa My
Life Today; “The Privilege of Prayer,” uk. loo kwenye kitabu kiitwacho Steps to
Christ; “This is Pure Religion” na “The Parable of the Good Samaritan,” sum ya
4 na ya 5 kwenye kitabu kiitwacho Welfare Ministiy.
Kum. 24:10—22
|
Kum. 24
10 Umkopeshapo jirani
yako cho chote kikopeshwacho usiingie katika nyumba yake kwenda kutwaa rehani
kwake.
11 Simama nje, yule umkopeshaye akuletee nje ile rehani. 12 Naye akiwa ni mtu maskini, usilale na rehani yake. 13 Sharti umrudishie rehani lichwapo jua, apate kulala na mavazi yake, na kukubarikia; nayo itakuwa ni haki kwako mbele za Bwana, Mungu wako. 14Usimwonee mtumishi mwenye ujira aliye maskini na uhitaji, kama ni wa nduguzo, au kama ni wageni wako mmojawapo walio katika nchi yako, ndani ya malango yako; 15 mpe ujira wake kwa siku yake, wala jua lisichwe juu yake; kwa maana ni maskini, moyo wake umeutumainia huo; asije akamlilia Bwana juu yako, ikawa ni dhambi kwako. 16 Mababa wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya baba zao; kila mtu na auawe kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe. 17 Usipotoshe hukumu ya mgeni, wala ya yatima; wala usitwae mavazi ya mjane, yawe rehani; 18 bali kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika Misri, Bwana, Mungu wako, akakukomboa huko; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili. 19 Uvunapo mavuno yako katika shamba lako, ukasahau mganda shambani, usirudi kuuchukua; na uwe wa mgeni, au yatima, au mjane; ili Bwana, Mungu wako, akubariki katika kazi yote ya mikono yako. 20 Utakapochuma matunda ya mizeituni yako, usirudi kuchuma mara ya pili; yaliyobaki apewe mgeni, na yatima, na mjane. 21 Uchumapo zabibu katika shamba lako la mizabibu, usichume mara ya pili; zilizobaki apewe mgeni, na yatima, na mjane. 22 Nawe kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili. |
Yon. 3
|
Yon. 3
1 Neno la Bwana
likamjia Yona mara ya pili, kusema,
2 Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru. 3 Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu. 4 Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa. 5 Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo. 6 Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu. 7 Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng'ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji; 8 bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake. 9 Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe? 10 Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende. |
Mal. 3:17
|
Mal. 3
17 Nao watakuwa wangu,
asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina
yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe
amtumikiaye.
|
Mat 15:32—38
|
Mat 15
32 Yesu akawaita
wanafunzi wake, akasema, Nawahurumia mkutano, kwa kuwa yapata siku tatu
wamekaa pamoja nami, wala hawana kitu cha kula, tena kuwaaga wakifunga
sipendi, wasije wakazimia njiani.
33 Wanafunzi wake wakamwambia, Tupate wapi mikate mingi hapa nyikani, hata kushibisha mkutano mkuu namna hii? 34 Yesu akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba, na visamaki vichache. 35 Akawaagiza mkutano waketi chini; 36 akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano. 37 Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate makanda saba, yamejaa. 38 Nao waliokula walikuwa wanaume elfu nne, bila wanawake na watoto. |
Marko. 6:34—44
|
Marko. 6
34 Naye aliposhuka
mashuani, akaona mkutano mkuu, akawahurumia; kwa sababu walikuwa kama kondoo
wasio na mchungaji; akaanza kuwafundisha mambo mengi.
35 Hata zilipopita saa nyingi za mchana, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na sasa kunakuchwa; 36 uwaage watu hawa, ili waende zao mashambani na vijijini kandokando, wakajinunulie chakula. 37 Akajibu, akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakamwambia, Je! Twende tukanunue mikate ya dinari mia mbili ili tuwape kula? 38 Akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Nendeni mkatazame. Walipokwisha kujua wakasema, Mitano, na samaki wawili. 39 Akawaagiza wawaketishe wote, vikao vikao, penye majani mabichi. 40 Wakaketi safu safu, hapa mia hapa hamsini. 41 Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akashukuru, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake wawaandikie; na wale samaki wawili akawagawia wote. 42 Wakala wote wakashiba. 43 Wakaokota vipande vilivyomegwa vya kuweza kujaza vikapu kumi na viwili; na vipande vya samaki pia. 44 Na walioila ile mikate wapata elfu tano wanaume. |
Gal. 6:2
|
Gal. 6
2 Mchukuliane mizigo
na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.
|
Ebr. 10:32—34
|
Ebr. 10
32 Lakini zikumbukeni
siku za kwanza, ambazo, mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano
makubwa ya maumivu;
33 pindi mlipotwezwa kwa mashutumu na dhiki, na pindi mliposhirikiana na wale waliotendewa hayo. 34 Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang'anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo. |
Wakati
wa mapumziko familia chache zikiwa na watoto wao wadogo zilijumuika pamoja
wakati wa siku kuu kutengeneza vifurushi vya vyakula na vifaa vya kuogea na kuwapatia
kwa watu wengi wasio na makazi kwenye mji wao. Baada ya kufanya kazi kwa saa
chache, walimgia kwenye magari yao na kwenda katikati ya mji na kwa muda wa
kama nusu saa hivi na walivigawa vita hivyo. Na baada ya hapo walikwenda kwenye
jumba la makumbusho na baada ya hapo walilcwenda kwa ajili ya chakula cha
jioni.Walipokuwa wanatembea kurudi kwenye magari yao mmoja wao alisema,
“Ninafurahi kuwa tumelitenda hili. Lakini je, mnatambua kuwa wengi wa wale
tuliowapatia chakula inawezekana kuwa sasa wana njaa tena?” Hakuna shaka, kule
nje kuna watu wengi wanaohitaji faraja, huruma, na msaada kiasi kwamba maweza
kuonekana kuwa ni hitaji kubwa kupita uwezo, hata kufikia hatua ya mtu kuweza
kufikiri: Kuna maana ganiya kufanya jambo lo lote? Ni kwa shida sana tunaweza
kupunguza tu! Yapo matatizo kadhaa kwa mtazamo huo wa kufikiri. Mosi, kama kila
mtu angefikiri namna hiyo,hakuna mtu ambaye angemsaidia mta ye yote, na
mahitaji, jinsii yalivyo ya kuogofya,yangelikuwa mabaya zaidi. Kwa upande
mwingine, kama mtu anayeweza kumsaidia mwingine angefanya hivyo, ndipo mahitaji
jinsi yalivyo ya kuogofya, yasingekuwa mabaya kiasi hicho. Pili, kamwe
hatujaambiwa kwenye Biblia kwamba, maumivu ya mwanadamu, mateso na uovu
vitaondolewa kabisa katika upande wetu huu wa mbingu.Na kwa kweli,
tulichoambiwa ni kmyume chake. Hata Yesu alipokuwa hapa duniani,hakuyatokomeza
mateso yote ya mwanadamu. Alifanya alichoweza. Sisi pia tunatakiwa kufanya
vivyo hivyo: kuleta faraja, huruma, na msaada kwa wale tunaoweza.
Maswali ya Kujadili:
1. Kanisa lako linawezaje
kufanywa kuwa mahali salama pa kuwaponyawaliovunjika moyo?
2. Ijadilini nukuu liii
katika darasa lenu: “Wengi hushangaa kwa nini Munguhachukui hatua. Mungu
anashangaa kwa nini wengi wa watu wake hawajali.”- Dwight Nelson, Pursuing
the Passion of Jesus (Nampa, Idaho:Pacific Press Publishing Association,
2005). Je, unakubaliana na wazo hili la changamoto? Kama ni hivyo, tutafanya
nini iii tuweze kubadilika?
3. Angalia nukuu hii kutoka
kwa Ellen G. White: “Maneno ya huruma yanayozungumzwa kwa usahili, na kujali
kidogo kunakotolewakwa usahili, utafukuzia mbali mawingu ya majaribu na
mashaka yanayojikusanya juu ya roho. Onesho la kweli la moyo ulio na huruma kama
ile ya Kristo, utakaotolewa kwa usahifi, una nguvu za kufungua milango ya
mioyo inayohitaji miguso sahili na laini ya Roho wa Kristo.” Ellen G. White,
Testmonies for the Church, vol. 9, uk. 30. Hili linatwambia nini juu ya nguvu
za ajabu za wema kwamba ukarimuna huruma vinavyoweza kuwa katika kuwafikia
watu na kuwasaidia wenye huzuni?
|
Maoni
Chapisha Maoni