TUNAWEZAJE KUITAMBUA IMANI YA KWELI KATIKATI YA DINI NA MADHEHEBU MENGI SANA ULIMWENGUNI LEO?
Vitabu
vyote vya dini hususani biblia na quran vinatambua na kukubaliana na ukweli
kuwa mitume na manabii ndio wanaotumika kuweka mwelekeo juu ya imani halisi ya
haki na ya kweli. Mafungu yafuatayo yanathibitisha nikisemacho
·
Ephesians 2:20Mmejengwa juu ya msingi wa
mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.
·
Quran
3:84. Sema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na
tuliyo teremshiwa sisi, na aliyo teremshiwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haak na
Yaakub na wajukuu zao, na aliyo pewa Musa na Isa na Manabii wengine kutoka kwa
Mola wao Mlezi. Hatubagui baina yao hata mmoja, na sisi ni wenye kusilimu
kwake.
·
Quran
10:19. Wala watu hawakuwa ila Umma mmoja tu.
Kisha wakakhitalifiana. Na lau kuwa si neno lililo kwisha tangulia kutokana na
Mola wako Mlezi, hapana shaka hukumu ingeli kwisha katwa baina yao katika hayo
wanayo khitalifiana.
·
Hii ina maana kwamba“Watu wote walikuwa na dini moja aliyokuja
nayo nabii Adam kisha wakahitilafiana” Na ndivyo isomekavyo pia katika
machapisho mengine ya Qur an.
·
Yeremiah 6:16 Bwana asema hivi, Simamenikatikanjiakuu, mkaone, mkaulize
habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katikanjia hiyo, nanyi
mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katikanjia hiyo.
Maandiko
haya yamefunua wazi kile nilichokisema kwamba manabii na mitume ndio njia ya
pekee na rahisi kwa kutuonyesha ndini ya kweli na sahihi.Tunamshukuru sana
Mungu kwa kutusaidia katika hili kwa sababu ingekuwa ni kazi ngumu kuliko
kupanda mlima mrefu sana kuitambua dini ya kweli na sahihi. Hili linatupa
uhakika wa kuipata dini ya kweli hata katika wimbi la dini na madhehebu mengi
sana ulimwenguni leo.
Andiko
lifuatalo linathibitisha zaidi dai hili;
Quran 42:13.
Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na
tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane
kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayo waitia. Mwenyezi Mungu humteua
kwake amtakaye, na humwongoa kwake aelekeaye. Linganisha na yeremia 6:17.
Hivyo
mapito sahihi ni katika njia ile ile waliyopita akina Ibrahimu,Musa,Isa na
manabii wengine wote maana maandiko yako bayana kwamba dini iliyoamrishwa ni
moja peke yake. Nitaonyesha baadae kidogo hawa manabii walishika njia ipi
katika kumwelekea Mungu ili tupate nuru kubwa na kuchuma maarifa ya kuitambua
imani sahihi. Tuihoji Qur an kama inatambua kuwepo kwa kundi la wakristo.
LIPO KUNDI LA WAKRISTO NA JE NI SAHIHI KUWEPO?
Quran 3:110. Nyinyi
mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza
maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini
ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu.
Quran 3:55.
Pale Mwenyezi Mungu alipo sema: Ewe Isa! Mimi nitakufisha, na nitakunyanyua
kwangu, na nitakutakasa na wale walio kufuru, na nitawaweka wale walio kufuata
juu ya wale walio kufuru, mpaka Siku ya Kiyama. Kisha marejeo yenu yatakuwa
kwangu, nikuhukumuni katika yale mliyo kuwa mkikhitalifiana.
Qur
an imeweka bayana uwepo wa kundi la wakristo ingawa inakiri kuwa wengi wao
walipotoka na hivyo kuiacha njia iliyo sahihi. Kilichonishangaza zaidi ndugu
zangu nikuona namna Qur an inavyoliweka kundi la wafuasi wa Yesu juu ya wote
mpaka siku ya mwisho.
Kama
mtu atakuwa ameweka itikadi yake pembeni na kutafakari kwa kina mambo haya
yazungumzwayo na vitabu hivi atakuwa ameanza kupata picha ya kile kisemwacho
ambao ni ukweli mtupu.
Biblia
inasema katika Matendo 11:26 kwamba“hata
alipokwisha kumwona akamletaAntiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima
wakakusanyika pamoja na kanisa nakuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwaWakristokwanza hapo Antiokia”.
Hivyo wafuasi wa
Bwana Yesu wanaitwa wakristo na ndio ambao kiukweli watawekwa juu ya wengine
wote mpaka siku ya kiama kama pia Qur an inavyiripoti. Kama hiyo haitoshi;
Katika Quran 41:61 msaafu unasema “Na
kwa hakika yeye ni alama ya Saa ya Kiyama. Basi usiitilie shaka, na nifuateni.
Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka”. Maneno kuwa yeye ni njia yanaungwa mkono pia
na Injili yake katika yohana 14:6 isemapo “Yesu akamwambia, Mimi
ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”.Hakuna alama nyingine ya saa ya
kiama.Chukua tahadhari mpendwa na ufanye maamuzi ya kweli na sahihi hata kama
ni kwa gharama kubwa.
Katika kile kinachosemwa na Qur
an kuhusu kuhitilafiana kwa wakristo, hata nabii Daniel alikiona na akasema
mamlaka ya pembe ndogo itaazimu kubadili majira na sheria.Kitabu cha Danieli 7
kinatoa unabii ya falme nne zilizowahi kutawala dunia;kwa macho ya kiroho
Danieli akionyeshwa kabla hazijatokea.Aliziona kwa mfano wa wanyama wanne ambao
ni simba,dubu,chui na mnyama wa kutisha.
Simba iliwakilisha Babeli, Dubu-Umedi na Uajemi,Chui-Ugiriki ama Uyunani na mnyama wa kutisha ni Rumi. Baada ya
Rumi kusambaratika katika mwaka wa 476 BK ndipo tukapata mataifa kumi, saba
yakiwepo mpaka leo na ndiyo
yanayotengeneza sehemu kubwa ya bara la
Ulaya(uingereza,ufaransa,ubeligiji,ujerumani,ureno,Hispania na Italia).Tatu
ziling’olewa kabisa(vandals,ostrogoth na heruli).
Kutoka
kwenye mataifa haya 10 ilitokea mamlaka nyingine ambayo ilikuwa tofauti na
zingine zote kwa kuwa hii ilikuwa na kinywa kilichonena maneno makuu ya
makufuru na hivyo kuonyesha kuwa ilikuwa na nguvu ya kidini maana kukufuru
kunahusiana na dini na siyo siasa.Kanisa katoliki na uongozi wake lilifanya
nikisemacho kwamba lilibadili majira na sheria za Mungu na hivyo ndio pembe
ndogo kama isemwavyo katika Dan.7:25.
ATAAZIMU KUBADILI MAJIRA NA SHERIA.
Amri za Mungu kama zisemwavyo na biblia
ni tofauti na zilivyoandikwa katika katekisimu zao.Amri ya pili
inayozuia kujifanyia sanamu za kuchonga imeondolewa, kisha wakaibadili amri ya
nne ya sabato na kusomeka shika kitakatifu siku ya Bwana.
Swali:
Hicho kitakatifu ni kinini? Siku ya Bwana ni ipi?. Katika biblia amri hiyo
inasema“Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku
sita fanya kazi, utende mambo yako yotelakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana,
Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti
yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala
mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu,
na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana
akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa”.Kama hiyo
haitoshi wakaigawa amri ya kumi inayozuia tamaa mara mbili ili kupata idadi
kamili ya amri 10 kwa kuwa wameiondoa amri ya pili!
Nithitibitisha
hili kwa kutumia vitabu vyao wenyewe.
·
No such law in the Bible
"Nowhere" in the bible do we find that Jesus or the apostles ordered
that the Sabbath be changed from Saturday to Sunday. We have the commandment of
God given to Moses to keep holy the Sabbath day, that is, the Seventh day of
the week, Saturday. Today, all Christians keep Sunday because it has been
revealed to us by the [Roman] church outside the Bible." Catholic Virginian, Oct. 3, 1947 (Hakuna sheria hiyo popote pale kwenye
biblia tunayoweza kupata kwamba Yesu au mitume waliamuru kubadilishwa kwa
sabato kutoka jumamosi kwenda jumapili.Tuna amri ya Mungu aliyompatia Musa
inayotutaka kuitakasa siku ya sabato,yaani siku ya saba ya wiki,jumamosi.Leo
wakristo wote huishika jumapili kwa sababu imefunuliwa kwetu na kanisa la katoriki,nje
ya biblia)
·
"You may read the Bible
from Genesis to Revelation, and you will not find a single line authorizing the
sanctification of Sunday. The Scriptures enforce the religious observance of
Saturday, a day which we never sanctified." James
Cardinal Gibbons, The Faith of Our Fathers (1917 ed.), pp.72,73.(Unaweza kusoma biblia
kutoka mwanzo mpaka ufunuo na hutapata msitari hata mmoja unaoidhinisha
utakaswaji wa jumapili.Maandiko yanaagiza kuitunza jumamosi,siku ambayo
hatukuitakasa)
·
"If protestants would
follow the Bible, they should worship God on the Sabbath Day, that is Saturday.
In keeping Sunday they are following a lawof the Catholic Church." Albert Smith, chancellor of the Archdiocese of Baltimore, replying
for the cardinal in a letter of Feb. 10, 1920.(Kama walokole wangefuata biblia,wanatakiwa
kumwabudu Mungu siku ya sabato,yaani jumamosi. Kwa kuitunza jumapili,wanafuata
sheria ya kanisa katoliki)
·
Peter Geiermann, C.S.S.R., The Converts Catechism of Catholic Doctrine (1957), p. 50.
"Question: Which is the Sabbath day?
"Answer: Saturday is the Sabbath day.
"Question: Why do we observe Sunday
instead of Saturday?
"Answer. We observe Sunday instead of
Saturday because the Catholic Church transferred the solemnity from Saturday to
Sunday."
·
Swali: Siku ya sabato ni ipi?
·
Jibu: Jumamosi ni siku ya sabato
·
Swali:Kwa nini tunaiadhimisha
jumapili badala ya jumamosi?
·
Jibu: Tunaadhimisha jumapili badala
ya jumamosi kwa sababu kanisa katoliki lilihamisha utukufu kutoka jumamosi
kwenda jumapili.MWISHO WA KUNUKUU.
Hapa sasa tunapata uhakika mwingine wa nani chanzo cha
kuhitilafiana kwa wakristo. Wakati wa Yesu na mitume watu wote walikuwa
wakiitunza sabato ya Bwana,siku ya saba yaani jumamosi.Taratibu taratibu
ukengeufu ukaanza kuingia kanisani na watu wakaanza kuiacha njia iliyonyoka ya
mapito ya mitume na manabii.
Ikawa watu wakaanza kuabudu jumamosi na jumapili na ilipofika
mwaka wa 321BK mfalme Constantine wa Rumi akatoa amri ya kuabudu siku ya
jumapili katika dola yake yote.Hapo ndipo kanisa katoliki linapopata nguvu.Hata
hivyo baadae waumini wa kanisa hili wakaanza kuhitilafiana tena kwa kile
ambacho kilionekana kuwa kiini macho kwa waumini.Kanisa lilifundisha na kuwataka watu kupokea msamaha
wa dhambi kutoka kwa papa huku hawaoni madai hayo kwenye biblia,ndipo watu Kama
Martin Luther walipoamua kujitenga na kanisa na wafuasi wake wakajiita
walutheri, Baadae tena waanglikan na madhehebu mengine mengi yakameguka.
Ndivyo kulivyo kumeguka na kuhitilafiana kwa makanisa kulivyotokea
kama inavyoripotiwa na Qur an pia kwamba walihitilafiana. Njia na mapito sahihi
ni ile ya zamani ambayo tumeiona kuwa ilikuwa ya mitume na manabii pia na
hakuna mabadiliko yatakayokuja kutokea. Sabato ilikuwepo tangu mwanzo wa
kuumbwa kwa sayari Dunia. Mwanzo 2:1-3 “1 Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi
lake lote. 2 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya;
akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. 3 Mungu
akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu
alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya”.
Hata kalenda ya kiarabu itumikayo kuhesabu siku kama itambuliwavyo
na waislamu inasaidia kuthibitisha kile nikisemacho na kuonyesha kuwa kweli
jumamosi ndiyo siku ya saba.
Jumapili:
yaum al-ahad (siku ya kwanza) يوم الأحد
Jumatatu:
yaum al-ithnayna (siku ya pili) يوم الإثنين
Jumanne:
yaum ath-thalatha (siku ya tatu) يوم الثلاثاء
Jumatano:
yaum al-arba`a (siku ya nne) يوم الأَربعاء
Alhamisi:
yaum al-khamis (siku ya tano) يوم خميس
Ijumaa:
yaum al-jum`a (siku ya mkutano) يوم الجمعة
Jumamosi:
yaum as-sabt (siku ya sabato)يوم السبت
Quran 3:71 inasema,
Enyi Watu wa Kitabu! Mbona kweli mnaivisha uwongo, na kweli mnaificha na hali
mnajua?
Hapa
inadhihirisha madai kuwa ni kweli sabato iligeuzwa na hawa wakristo waliokuwa wanajua
ukweli ila wakaamua kuuvisha uongo.Ili kupona kwao kuje wanatakiwa kuyarejea
mapito ya zamani ya mitume na manabii ya kuabudu na kuitunza sabato ya Bwana
kama ilivyoamuriwa na vitabu vyote vya dini hizi.Hili pia linathibitishwa na
fungu lifuatalo;
Quran 5: 68.
Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Hamna lenu jambo mpaka muishike Taurati na Injili na
yote mlio teremshiwa kutokana na Mola wenu Mlezi. Na hakika ulio teremshiwa
wewe kutokana na Mola wako Mlezi yatawazidishia wengi katika wao uasi na
ukafiri. Basi usiwasikitikie watu makafiri.
Baada ya mpasuko wa hawa wakristo,kuna
wapo waliobaki imara?
Quran 9:29. Piganeni
na wasio muamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho, wala hawaharimishi alivyo
harimisha Mwenyezi Mungu na Mtume, wala hawashiki Dini ya Haki, miongoni mwa
walio pewa Kitabu, mpaka watoe kodi kwa khiari yao, hali wamet'ii.
Hapa
jambo linawekwa sawa kwamba kuna miongoni mwa waliopewa kitabu(wakristo) ambao
hawaharimishi alivyoharamisha mwenyezi Mungu.Hii inaonyesha si wote,kumbe kuna
waliobakia kuwa waaminifu.Amri hii ilitolewa na Abubaker alipokuwa ameyakusanya
makabila ya kiarabu kwa ajili ya vita dhidi ya rumi ya mashariki waliambiwa
kudhuru wote waabudu sanamu na kuwaacha wote wacha Mungu wa kweli.Na hili ndilo
kundi ambalo nalizungumzia kuwa wametunza maagizo ya Bwana tangu zamani. Ukweli
ni kwamba kwenye kila kizazi, kumekuwepo waaminifu wa kweli ambao wamezitunza
amri zote 10 za Mungu kwa gharama yoyote ile. Wengi walimwaga damu kwa kuwa
watiifu kwa Mungu.
Rumi
ya kidini chini ya uongozi wa upapa kuanzia mwaka 538 BK mpaka 1798 BK
ilitawala dunia na kuua mamilioni ya watu waliopingana na mafundisho yake.Historia
inaonyesha kwamba zaidi ya watu milioni 50 waliuawa na mkono huu.Hakuna mauaji
yaliyowahi kufanyika kama haya tangu kuwepo kwa dunia.Kipindi hiki kinaitwa
DARK AGE na biblia ilipigwa marufuku kusomwa wala kuuzwa. Nitaeleza habari hizi
zaidi katika waraka wangu mwingine.
DINI YA MITUME NA MANABII NI IPI SASA?
Tangu
mwanzo,manabii na mitume wote wamekuwa wakiishika na kuitunza sabato ya
Bwana.Sabato ni amri ya Mungu aliyoitoa mwenyewe,akaiandika kwa chanda chake
mwenyewe na nabii Ibrahimu akashika amri za Mungu ikiwepo nah ii pia.Mwanzo
26:5 inasema “Kwa sababu Ibrahimu
alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu
zangu, na sheria zangu”. Napa Ibrahimu aliitii sabato kwa sababu
Mungu asingesema kuwa alihifadhi sheria zake kama angevunja hata iliyo moja.
Yakobo anatusaidia katika hili kwamba ukivunja amri 1, umevunja zote(yakobo 2:10)-Maana mtu awaye yote
atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.Hivyo ni kusema
Ibrahimu alizishika sheria na amri zote za Mungu ikiwepo ya sabato.
MUSA-huyu ndiye mpokeaji wa amri zote.Baada ya Mungu kuziandika kwa
chanda chake mwenyewe alimkabidhi Musa kuwafikishia wana wa Israel na hakuna
shaka kuwa nabii huyu alikuwa mtiifu wa amri za Mungu ikiwepo na SABATO.( Kumbukumbu la torati
4:13 Akawahubiri agano
lake, alilowaamuru kulitenda, yaani, zile amri kumi; akaziandika juu ya mbaombili za mawe)
Kumbukumbu la
torati 5:22 Haya ndiyo maneno
ambayo Bwana aliwaambia mkutano wenu wote mlimani kwa sauti kuu toka kati ya
moto, na wingu, na giza kuu; wala hakuongeza neno. Akayaandika juu ya mbaombili za mawe, akanipa.
Matendo 15:21 Kwa maana tangu zamani
za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila
sabato katika masinagogi. Ni wazi kabisa kwamba kumbe sabato imekuwepo tangu
zamani na manabii waliitii.
YESU(ISA )-Huyu nae ilikuwa desturi yake kuishika
sabato kama inavyowekwa bayana katika luka 4:16 ikisema Akaenda Nazareti, hapo
alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi
yake, akasimama ili asome.Desturi ni kawaida au tamaduni.ilikuwa hivyo
kwake siku zote.
Matendo 13:27 Kwa maana wakaao
Yerusalemu, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua yeye, wala maneno ya manabii
yanayosomwa kila sabato, wameyatimiza kwa kumhukumu. Kumbe manabii waliizingatia sabato
kama lisemavyo fungu hili kwa uwazi kabisa.
MITUME WA YESU VIPI?
·
Matendo 16:13 Hata siku ya sabato tukatoka nje ya
lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali;
tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale
·
Matendo 17:2 Na Paulo, kama
ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya
maandiko sabato tatu
·
Matendo 18:4 Akatoa hoja zake
katika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani
·
Matendo 13:14 Lakini wao wakatoka
Perge, wakapita kati ya nchi, wakafika Antiokia, mji wa Pisidia, wakaingia
katika sinagogi siku ya sabato, wakaketi.
Mafungu haya yote
yanaonyesha namna ambavyo mitume walikuwa wakiitunza sabato ya Bwana.Wewe vipi
mpendwa?
Kuthibitisha zaidi
kuwa sabato iliheshimiwa tangu zamani, hata Quran ilipokuja ililipoti kitu
hicho.
Quran 7: 163.
Na waulize khabari za mji ulio kuwa kando ya bahari, wakiivunja Sabato
(Jumaamosi ya mapumziko). Samaki walikuwa wakiwajia juu juu siku ya mapumziko
yao, na siku zisio kuwa za kupumzika hawakuwa wakiwajia. Kwa namna hiyo
tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakifanya upotovu.
Kutoka 20:8-11(Ikumbuke siku ya Sabato
uitakase.Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote lakini siku ya saba ni
Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana
wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa
kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.Maana, kwa siku sita Bwana
alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya
saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa).
Quran 4:47
Enyi mlio pewa Kitabu! Aminini tuliyo yateremsha yenye kusadikisha yale mliyo
nayo, kabla hatujazigeuza nyuso tukazipeleka kisogoni, au tukawalaani kama
tulivyo walaani watu wa Sabato (Jumaamosi). Na amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima
ifanyike.
Waliolaaniwa
ni wale walioivunja sabato na ndio maana katika fungu lifuatalo likasisitiza
hicho;
Quran 2:65.
Na hakika mlikwisha yajua ya wale miongoni mwenu walio ivunja Sabato,(siku ya
mapumziko, Jumaa Mosi) na tukawaambia:Kuweni manyani wadhalilifu.
Kiukweli sioni lugha ngumu na kali
kama hii iliyotumika kuwaita wavunja sabato ya Bwana na pia sioni ugumu wa moyo
wa yeyote Yule kuendelea kuipinga sabato ya Bwana.Fanya maamuzi ya kweli ndugu
yangu tuokolewe.Suala la wokovu ni la mtu mwenyewe siyo familia wala rafiki
maana kila mtu atasimama mwenyewe siku ya hukum
Quran 4:154.
Na tukanyanyua mlima juu yao kwa kufanya agano nao. Na tukawaambia: Ingilieni
mlangoni kwa unyenyekevu. Na tukawaambia: Msiivunje Siku ya Sabato (Jumaa
mosi). Na tukachukua kwao ahadi iliyo madhubuti.
Quran 16:124.
Hakika siku ya Sabato (Jumaamosi) waliwekewa wale walio khitalifiana kwa ajili
yake. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka atahukumu baina yao Siku ya
Kiyama katika yale waliyo kuwa wakikhitalifiana
IJUMAA IMETOKA WAPI?
Quran 17: 77.
Huo ndio mwendo kwa Mitume tulio watuma kabla yako. Wala hupati mabadiliko
katika mwendo wetu.linganisha pia na quran 3:84 tuliyokwisha kuiona.
Hapa
tunaona kuwa mabadiliko ya mitume si kigezo cha kubadili mafunuo na amri za
Mungu.Zingatia sentensi iliyopigiwa mstari hapo juu.
Historia
inaonyesha kwamba mtume Mohammad alikuwa akifanya sala kwa kuangalia upande wa
Yerusalemu(Baytil Muqaddas) kwa muda wa mwaka mmoja na nusu.Inaonyesha kuwa
alikuwa akiijua vizuri dini ya kikristo kwa kuwa hata akina Danieli walifanya
hivyo.Soma fungu hili;
Quran 2: 144.
Kwa yakini tukiona unavyo geuza geuza uso wako mbinguni. Basi tutakuelekeza
kwenye Kibla ukipendacho. Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu; na
popote mnapokuwa zielekezeni nyuso zenu upande huo; na hakika wale walio pewa
Kitabu wanajua kwamba hiyo ni haki itokayo kwa Mola wao Mlezi. Na Mwenyezi
Mungu si mwenye kughafilika na yale wanayo yatenda.Danieli 6:10 inasema Hata Danieli, alipojua
ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na
madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;)
akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake,
kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
Katika
pango la jabal ilaa mwaka wa 610 BK ndipo mabadiliko mengi yakaja kwa mtume
ikiwepo na sala ya ijumaa ambayo ilianza rasmi mwaka 622BK
Quran 2: 145.
Na hao walio pewa Kitabu, hata ukiwaletea hoja za kila namna, hawatafuata Kibla
chako; wala wewe hutafuata kibla chao, wala baadhi yaohawatafuata kibla cha
wengineo; na kama ukiyafuata matamanio yao baada ya kukufikia ujuzi, hakika
hapo utakuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.
Mtume
kwa mara ya kwanza aliswali swala ya ijumaa katika maskani ya Bani Salim bin
Awf katika wangwa wa Ronunaa.Alikuwa katika safari yake kwenda madina akitokea
makka.
Ibada
ya ijumaa haibebi sifa ya jumamosi na hata hivyo imetajwa mara moja tu katika
Qur an nzima napo ikiwa haikatazi kabisa kufanya kazi siku hiyo, lakini
jumamosi ni siku ya kuadhimisha matendo ya ibada tu.Tuisome iyo aya;Quran 62:9-10 inasema Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya
Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara.
Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua.
10.
Na itakapo kwisha Sala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi
Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa.
Unaona?
Haijakataza kufanya kazi ilihali Mungu alitupatia kielelezo cha namna ya
kuenenda kupitia kazi yake ya uumbaji; Kwamba aliumba kwa siku sita kasha
akapumzika kama ilivyosemwa katika biblia lakini pia katika Qur an 7:54 Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu
na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika
usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazo tumika
kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi
Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote. Soma pia
KUTOKA 20:11 uone kufanana kwake.
Wapo watu wasemao kuwa amri ya sabato iliwahusu wayahudi peke
yao! Nami nauliza swali?
·
Je, kuiba,kusema uongo,
kuzini, kutokuwaheshimu wazazi kunaruhusiwa leo kwa kuwa hizi nazo zilikuwa za
wayahudi?
·
Ina maana gani yesu
kusema katika marko 2:27 kwamba sabato ilifanyika kwa ajili ya wanadamu?
Ukweli
ni kwamba watu wanajifariji tu kwa madai haya.Ukweli utaendelea kudumu mpaka
mwisho wa wakati.Amri ya sabato ni mhuri wa Mungu mwenyewe.Ni ishara ya
utakaso, ukombozi na mamlaka yake ya uumbaji.
SABATO ITADUMU MILELE.HATA MBINGUNI ITATUNZWA KWA
KICHO SANA NA VIUMBE VYOTE (ISAYA 66:22-24).
IMESALIA RAHA YA SABATO KWA WATU WA MUNGU.
Isikie sauti ya Mungu usiwe mtu mwenye masikio
asiyesikia. Mungu awatangulie mtafakaripo maneno haya ya uzima.AMEN!
Nimetumia Biblia, Qur an na vitabu vingine vya dini
pamoja na vya historia kuuthibitisha ukweli huu ambao watu wengi hawapendi
kuusema. Msaafu wa Qur an umeweka bayana sana suala hili kama ilivyo kwa biblia
pia.
KUMBUKA DUNIA INA MWISHO WAKE.YESU ANAKUJA TENA.YEYE
NI SAA YA ALAMA YA KIAMA.
Maoni
Chapisha Maoni