Ufunuo wa Yohana
Kulikuwa na Vita Mbinguni;Mikaeli na Malaika zake wakapigana na yule joka,yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;nao hawakushinda,wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
Yule joka akatupwa,nyoka
wa zamani,aitwaye ibilisi na shetani,audanganyaye ulimwengu wote;akatupwa hata
nchi,na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Nikasikia
sauti kuu mbinguni,ikisema,Sasa kumekuwa wokovu,na nguvu,na ufalme wa Mungu
wetu,na mamlaka ya Kristo wake;kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu,yeye
awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.Nao wakamshinda kwa damu ya
mwana kondoo,na kwa neno la ushuhuda wao,ambao hawakuyapenda maisha yao hata
kufa.
Kwa hiyo shangilieni,enyi mbingu,nanyi mkaao
humo.Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule ibilisi ameshuka kwenu mwenye
ghadhabu nyingi akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
Na joka
yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi,alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa
mtoto mwanaume.
Mwanamke
yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa ,ili aruke,aende zake nyikani
hata mahali pake,hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati,mbali
na nyoka huyo.
Nyoka
akatoa katika kinywa chake ,nyuma ya huyo mwanamke,maji kama mto,amfanye
kuchukuliwa na mto ule.
Nchi
ikamsaidia mwanamke;nchi ikafunua kinywa chake,ikaumeza mto ule alioutoa yule
joka katika kinywa chake.Joka akamkasilikia yule mwanamke,akaenda zake afanya
vita juu ya wazao wake waliosalia,wazishikao amri za Mungu,na kuwa na ushuhuda
wa Yesu;naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.
Nukuu yote
hii imetoka Ufunuo 12,fungu la 7 hadi 17
Inaeleza
kulikuwa na Vita Mbinguni kati ya
Miakaeli(Yesu) na malaika zake wakapigana na shetani na malaika zake(mapepo).Imeeleza
Shetani hakushinda sabubu yeye ndiyo alianzisha hiyo vita,Mbinguni kulikuwa
amani yeye ndiyo alianzisha vita;
Fundisho
fupi kidogo” Inaweza kukawepo amani katika familia,taasisi,kikundi fulani
lakini akatokea mtu akaanzisha kitu cha kuleta mvurugano,hiyo tabia aliasisi
shetani”
Shetani alishindwa hiyo vita akatupwa chini.Shetani
alipapenda sana mbinguni ndiyo maana alikasilika sana kutupwa chini.Wanadamu
tunaonywa Shetani alishuka mwenye ghadhabu nyingi anafanya kazi kwa bidii ya
kuteka wanadamu akijua muda wake ni mchache tu.
Shetani alipoona ya kuwa ametupwa alimkasilikia mwanamke
aliye mzaa mtoto Mwananume.
Maana ya
mwanamke Ni kanisa.
Mtoto
mwanaume –Ni Yesu Kristo.
Kanisa
lenye kushika amri za Mungu zote na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo ndiyo
alianza kupambana nalo Ibilisi ili watu wengi wasiende mbinguni alikofukuzwa
yeye.
Kazi yake
ni kuharibu mipango ya Bwana,Mungu wetu.
Nyoka
akatoa katika kinywa chake ,nyuma ya huyo mwanamke,maji kama mto,amfanye
kuchukuliwa na mto ule.
Maana yake ni kwamba shetani akatoa mafundisho ya uongo.Hapa
ndipo chimbuko la dini nyingi nyingi duniani ili ukweli usijulikane ni
upi.Lengo lake ni kuwa mafundisho ya uongo yaumeze ukweli.Aliona kupambana na
Imani ya Kikristo ni kujifanaisha nayo.Hapa ndipo unapata wahubiri wanaenda
kupata nguvu za kufanya ishara kwa shetani,kutoa pepo na kadharika.Ukiwakuta
kwenye jukwaa wanamhubiri Kristo,Kumbe ni mawakala wa shetani.
Mungu alilisaidia kanisa lake ili ukweli usipotee,ndiyo maana
mpaka leo ukweli upo bayana na udanganyifu wa shetani upo bayana.
“akaenda
zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia,wazishikao amri za Mungu,na kuwa
na ushuhuda wa Yesu;naye akasimama juu ya mchanga wa bahari”
Shetani anafanya vita na wazao wa mwanamke waliosalio(maana
yake ni wachache waujuao ukweli)
Wazishikao amri za Mungu na kuwa na ushuhuda wa Kristo.
Makanisa mengi yanaushuhuda wa Yesu tu pasipo kuzishika amri
za Mungu zote alizopewa Nabii Musa.
Masalia Wa Mungu ni wale Wazishikao amri za Mungu na kuwa na Ushuhuda Wa Yesu Kristo.
Amri za Mungu zinapatikana katika Kitabu cha Kutoka 20
1. Usiwe na
Miungu mingine ila mimi
2. Usijifanyie
sanamu ya kuchonga wala mfano wa kitu chochote kilicho juu Mbinguni,wala
kilicho duniani,walakilcho majini chini ya dunia.Usivisujudie wala kuvitumikia
3. Usilitaje
bure jina la Bwana ,Mungu wako.
4. Ikumbuke
siku ya sabato uitakase.Siku sita fanya kazi utende mambo yako yote.lakini siku
ya saba ni sabato ya Bwana,Mungu Wako.(Lengo la kushika sabato ni kufanya
kumbukumbu kwamba Mungu ndiye aliyeiumba dunia.Laiti wanadamu wangeishika hii
amri ingewakumbusha wao wameumbwa na Bwana ,Mungu wao na kila kitu wanachokiona
kimetokana na Mungu na maisha yao binafsi yametoka kwa Mungu )
5. Waheshimu
baba yako na mama yako;siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi.
6. Usiue
7. Usizini
8. Usiibe
9. Usimshuhudie
jirani yako uongo
10. Usiitamani
nyumba ya jirani yako,usimtamani mke wa jirani yako;wala mtumwa wake,wala
mjakazi wake,wala ng’ombe wake,wala punda wake,wala usitamani chochote alicho
nacho jirani yako.
Walimwengu wengi hawaishiki amri ya
nne.
“naye akasimama juu ya mchanga wa bahari”
Mchanga
wa bahari ni watu wengi.
Shetani
akasimamama juu ya mchanga wa bahari-maana yake ni watu wengi wanayafuata
mafundisho Yake.
Hii
inafana na pale aliposema Yesu Kristo “Njia ya kwenda upotevuni ni pana na ni
wengi waipitao na njia yakwenda Uzimani
ni nyembamba na ni wachache waionayo”
Maoni
Chapisha Maoni