Januari 26 - Mungu au Sanamu?
Mungu au Sanamu? Sanamu zao ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu... Wazfanyao watafanana nazo, Kila mmoja anayezitumainia. Zaburi 115:4-8. Siku za Nuhu laana maradufu ilikuwa duniani ikiwa ni matokeo ya uasi wa Adamu na ya mauaji yaliyofanywa na Kaini. Hata hivyo, haya yalikuwa hayajabadilisha sana uso wa asili wa dunia. . . jamiii ya binadamu bado ilikuwa katika nguvu zake za awali. Vizazi vichache tu vilikuwa vimepita tangu Adamu alipoweza kuufikia mti ambao ulikuwa na uwezo wa kurefusha uhai; na urefu wa maisha ya mwanadamu ulikuwa bado ukipimwa kwa karne. Kama watu hawa walioishi maisha marefu wakiwa na nguvu zisizo za kawaida katika kupanga na kutenda, wangejitoa wenyewe kwa ajili ya utumishi wa Mungu, wangefanya jina la Muumba wao liwe sifa katika dunia... Lakini walishindwa kufanya hili. ... Wakiwa hawakutamani kumfanya Mungu abaki katika ujuzi wao, wakafikia hatua ya kukana kuwepo kwake. Wakatukuza viumbe ...