Kuwahubiri wauaji Sehemu ya II-Somo toka Rwanda

Na Fodidas Ndamyumugabe Kumbuka: Fodidasi amekamatwa na wauaji, waliomwamuru ajichimbie kaburi lake mwenyewe. Kadri aliyochimba kaburi, mmoja wa wauaji hao alivutiwa na Biblia ya Fodidasi na kuanza kumwuliza maswali. Mara baada ya kaburi kuchimbwa ,kundi hilo la wauaji liliamua kutumia kaburi hilo kumzika mtu mwingine. Kabla ya kumwamuru Fodidasi kuchimba kaburi la pili, walimpatia wasaa apate kuwahubiri. Kwanza ninawashukuru sana. “Ahsanteni kwa kufanya dua kwa ajili ya mtu mliyemwua. Hata hivyo mwapaswa mjue Biblia isemacho kuhusu kifo—wasaa pekee ambapo waweza kuokolewa ni wakati ukingali hai—siyo baada ya kifo. “ Kwa sababu walio hai wanajua kuwa watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote ” Mhubiri 9:5. “Sitawasihi kuwa mniachie hai,” aliendelea kujieleza, “kwa sababu najua hata mkiniua muda utafika ambapo nitafufuliwa.” “Miongofli mwa watu mnaowaua ni wa makabila mengine—siyo Wahutu au Watusi. Ni watoto wa Mungu. Mnafikiri mnapambana vita ya kikabila, ila mmekosea. H...