TUNAWEZAJE KUITAMBUA IMANI YA KWELI KATIKATI YA DINI NA MADHEHEBU MENGI SANA ULIMWENGUNI LEO?
Vitabu vyote vya dini hususani biblia na quran vinatambua na kukubaliana na ukweli kuwa mitume na manabii ndio wanaotumika kuweka mwelekeo juu ya imani halisi ya haki na ya kweli. Mafungu yafuatayo yanathibitisha nikisemacho · Ephesians 2:20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. · Quran 3:84 . Sema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na tuliyo teremshiwa sisi, na aliyo teremshiwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haak na Yaakub na wajukuu zao, na aliyo pewa Musa na Isa na Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi. Hatubagui baina yao hata mmoja, na sisi ni wenye kusilimu kwake. · Quran 10:19 . Wala watu hawakuwa ila Umma mmoja tu. Kisha wakakhitalifiana. Na lau kuwa si neno lililo kwisha tangulia kutokana na Mola wako Mlezi, hapana shaka hukumu ingeli kwisha katwa baina yao katika hayo wanayo khitalifiana....